(SWAHILI) QURAN SURE SEÇİNİZ
(SWAHILI) QURAN |
| 100 - AL - A'ADIYAAT |
| KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
|
| 1. | Naapa kwa farasi wendao mbio wakipumua, |
| 2. | Na wakitoa moto kwa kupiga kwato zao chini, |
| 3. | Wakishambulia wakati wa asubuhi, |
| 4. | Huku wakitimua vumbi, |
| 5. | Na wakijitoma kati ya kundi, |
| 6. | Hakika mwanaadamu ni mtovu wa fadhila kwa Mola wake Mlezi! |
| 7. | Na hakika yeye mwenyewe bila ya shaka ni shahidi wa hayo! |
| 8. | Naye hakika bila ya shaka ana nguvu za kupenda mali! |
| 9. | Kwani hajui watakapo fufuliwa waliomo makaburini? |
| 10. | Na yakakusanywa yaliomo vifuani? |
| 11. | Kuwa hakika Mola wao Mlezi siku hiyo bila ya shaka atakuwa na khabari zao wote! |