(SWAHILI) QURAN |
96 - AL - A'LAQ |
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
1. | Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba, |
2. | Amemuumba binaadamu kwa tone la damu, |
3. | Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote! |
4. | Ambaye amefundisha kwa kalamu. |
5. | Kamfundisha mtu aliyo kuwa hayajui. |
6. | Kwani! Hakika mtu bila ya shaka huwa jeuri |
7. | Akijiona katajirika. |
8. | Hakika kwa Mola wako Mlezi ndio marejeo. |
9. | Umemwona yule anaye mkataza |
10. | Mja anapo sali? |
11. | Umeona kama yeye yuko juu ya uwongofu? |
12. | Au anaamrisha uchamngu? |
13. | Umeona kama yeye akikanusha na anarudi nyuma? |
14. | Hajui ya kwamba Mwenyezi Mungu anaona? |
15. | Kwani! Kama haachi, tutamkokota kwa shungi la nywele! |
16. | Shungi la uwongo, lenye makosa! |
17. | Basi na awaite wenzake! |
18. | Nasi tutawaita Mazabania! |
19. | Hasha! Usimt'ii! Nawe sujudu na ujongee! |