1. |
Litakase jina la Mola wako Mlezi aliye juu kabisa,
|
2. |
Aliye umba, na akaweka sawa,
|
3. |
Na ambaye amekadiria na akaongoa,
|
4. |
Na aliye otesha malisho,
|
5. |
Kisha akayafanya makavu, meusi.
|
6. |
Tutakusomesha wala hutasahau,
|
7. |
Ila akipenda Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye anayajua yaliyo dhaahiri na yaliyo fichikana.
|
8. |
Na tutakusahilishia yawe mepesi.
|
9. |
Basi kumbusha, kama kukumbusha kunafaa.
|
10. |
Atakumbuka mwenye kuogopa.
|
11. |
Na atajitenga mbali nayo mpotovu,
|
12. |
Ambaye atauingia Moto mkubwa.
|
13. |
Tena humo hatakufa wala hawi hai.
|
14. |
Hakika amekwisha fanikiwa aliye jitakasa.
|
15. |
Na akakumbuka jina la Mola wake Mlezi, na akasali.
|
16. |
Lakini nyinyi mnakhiari maisha ya dunia!
|
17. |
Na Akhera ni bora na yenye kudumu zaidi.
|
18. |
Hakika haya yamo katika Vitabu vya mwanzo,
|
19. |
Vitabu vya Ibrahimu na Musa.
|