(SWAHILI) QURAN |
90 - AL - BALAD |
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
1. | Naapa kwa Mji huu! |
2. | Nawe unaukaa Mji huu. |
3. | Na naapa kwa mzazi na alicho kizaa. |
4. | Hakika tumemuumba mtu katika taabu. |
5. | Ati anadhani hapana yeyote ataye muweza? |
6. | Anasema: Nimeteketeza chungu ya mali. |
7. | Ati anadhani ya kuwa hapana yeyote anaye mwona? |
8. | Kwani hatukumpa macho mawili? |
9. | Na ulimi, na midomo miwili? |
10. | Na tukambainishia zote njia mbili? |
11. | Lakini hakujitoma kwenye njia ya vikwazo vya milimani. |
12. | Na nini kitakujuvya ni nini njia ya vikwazo vya milimani? |
13. | Kumkomboa mtumwa; |
14. | Au kumlisha siku ya njaa |
15. | Yatima aliye jamaa, |
16. | Au masikini aliye vumbini. |
17. | Tena awe miongoni mwa walio amini na wakausiana kusubiri na wakausiana kuhurumiana. |
18. | Hao ndio watu wa kheri wa kuliani. |
19. | Lakini walio zikataa Ishara zetu, hao ndio watu wa shari wa kushotoni. |
20. | Juu yao utakuwa Moto ulio fungiwa kila upande. |