(SWAHILI) QURAN SURE SEÇİNİZ
(SWAHILI) QURAN |
| 104 - AL - HUMAZAH |
| KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
|
| 1. | Ole wake kila safihi, msengenyaji! |
| 2. | Aliye kusanya mali na kuyahisabu. |
| 3. | Anadhani ya kuwa mali yake yatambakisha milele! |
| 4. | Hasha! Atavurumishwa katika H'ut'ama. |
| 5. | Na nani atakujuvya ni nini H'ut'ama? |
| 6. | Moto wa Mwenyezi Mungu ulio washwa. |
| 7. | Ambao unapanda nyoyoni. |
| 8. | Hakika huo utafungiwa nao |
| 9. | Kwenye nguzo zilio nyooshwa. |