1. |
Itapo chanika mbingu,
|
2. |
Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza,
|
3. |
Na ardhi itakapo tanuliwa,
|
4. |
Na kuvitoa vilivyo kuwa ndani yake, ikawa tupu,
|
5. |
Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza,
|
6. |
Ewe mtu! Hakika wewe unajikusuru kwa juhudi kumwendea Mola wako Mlezi, basi utamkuta.
|
7. |
Ama atakaye pewa daftari lake kwa mkono wa kulia,
|
8. |
Basi huyo atahisabiwa hisabu nyepesi,
|
9. |
Na arudi kwa ahali zake na furaha.
|
10. |
Na ama atakaye pewa daftari lake kwa nyuma ya mgongo wake,
|
11. |
Basi huyo ataomba kuteketea.
|
12. |
Na ataingia Motoni.
|
13. |
Hakika alikuwa furahani kati ya jamaa zake.
|
14. |
Huyo hakika alidhani kuwa hatarejea tena.
|
15. |
Kwani? Hakika Mola wake Mlezi alikuwa akimwona!
|
16. |
Basi ninaapa kwa wekundu wa jua linapo kuchwa,
|
17. |
Na kwa usiku na unavyo vikusanya,
|
18. |
Na kwa mwezi unapo pevuka,
|
19. |
Lazima mtapanda t'abaka kwa t'abaka!
|
20. |
Basi wana nini hawaamini?
|
21. |
Na wanapo somewa Qur'ani hawasujudu?
|
22. |
Bali walio kufuru wanakanusha tu.
|
23. |
Na Mwenyezi Mungu anajua wanayo yadhamiria.
|
24. |
Basi wabashirie adhabu chungu!
|
25. |
Isipo kuwa wale walio amini na wakatenda mema; hao watakuwa na ujira usio malizika.
|