1. |
Naapa kwa usiku unapo funika!
|
2. |
Na mchana unapo dhihiri!
|
3. |
Na kwa Aliye umba dume na jike!
|
4. |
Hakika juhudi zenu bila ya shaka ni mbali mbali.
|
5. |
Ama mwenye kutoa na akamchamngu,
|
6. |
Na akaliwafiki lilio jema,
|
7. |
Tutamsahilishia yawe mepesi.
|
8. |
Na ama mwenye kufanya ubakhili, na asiwe na haja ya wenzake,
|
9. |
Na akakanusha lilio jema,
|
10. |
Tutamsahilishia yawe mazito!
|
11. |
Na mali yake yatamfaa nini atapo kuwa anadidimia?
|
12. |
Hakika ni juu yetu kuonyesha uwongofu.
|
13. |
Na hakika ni yetu Sisi Akhera na dunia.
|
14. |
Basi nakuonyeni na Moto unao waka!
|
15. |
Hatauingia ila mwovu kabisa!
|
16. |
Anaye kadhibisha na kupa mgongo.
|
17. |
Na mchamngu ataepushwa nao,
|
18. |
Ambaye hutoa mali yake kwa ajili ya kujitakasa.
|
19. |
Na wala si kwa kuwa yupo yeyote aliye mfanyia hisani ndio anamlipa.
|
20. |
Ila ni kutaka radhi ya Mola wake Mlezi aliye juu kabisa.
|
21. |
Naye atakuja ridhika!
|