(SWAHILI) QURAN SURE SEÇİNİZ
(SWAHILI) QURAN |
| 111 - AL - MASAD |
| KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
|
| 1. | Imeangamia mikono ya Abu Lahab, na yeye pia ameangamia. |
| 2. | Hayatamfaa mali yake, wala alivyo vichuma. |
| 3. | Atauingia Moto wenye mwako. |
| 4. | Na mkewe, mchukuzi wa kuni, |
| 5. | Shingoni mwake iko kamba iliyo sokotwa. |