(SWAHILI) QURAN SURE SEÇİNİZ
(SWAHILI) QURAN |
101 - AL - QAARIA'H |
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
1. | Inayo gonga! |
2. | Nini Inayo gonga? |
3. | Na nini kitacho kujuilisha nini Inayo gonga? |
4. | Siku ambayo watu watakuwa kama nondo walio tawanyika; |
5. | Na milima itakuwa kama sufi zilizo chambuliwa! |
6. | Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito, |
7. | Huyo atakuwa katika maisha ya kupendeza. |
8. | Na yule ambaye mizani yake itakuwa khafifu, |
9. | Huyo maskani yake yatakuwa Moto wa Hawiya! |
10. | Na nini kitacho kujuilisha nini hiyo? |
11. | Ni Moto mkali! |