(SWAHILI) QURAN SURE SEÇİNİZ
(SWAHILI) QURAN |
| 97 - AL - QADR |
| KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
|
| 1. | Hakika Sisi tumeiteremsha Qur'ani katika Laylatul Qadri, Usiku wa Cheo Kitukufu. |
| 2. | Na nini kitacho kujuulisha nini Laylatul Qadri? |
| 3. | Laylatul Qadri ni bora kuliko miezi elfu. |
| 4. | Huteremka Malaika na Roho katika usiku huo kwa idhini ya Mola wao Mlezi kwa kila jambo. |
| 5. | Amani usiku huo mpaka mapambazuko ya alfajiri. |