(SWAHILI) QURAN SURE SEÇİNİZ
(SWAHILI) QURAN |
91 - ASH-SHAMS |
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
1. | Naapa kwa jua na mwangaza wake! |
2. | Na kwa mwezi unapo lifuatia! |
3. | Na kwa mchana unapo lidhihirisha! |
4. | Na kwa usiku unapo lifunika! |
5. | Na kwa mbingu na kwa aliye ijenga! |
6. | Na kwa ardhi na kwa aliye itandaza! |
7. | Na kwa nafsi na kwa aliye itengeneza! |
8. | Kisha akaifahamisha uovu wake na wema wake, |
9. | Hakika amefanikiwa aliye itakasa, |
10. | Na hakika amekhasiri aliye iviza. |
11. | Kina Thamudi walikadhibisha kwa sababu ya upotofu wao, |
12. | Alipo simama mwovu wao mkubwa, |
13. | Hapo Mtume wa Mwenyezi Mungu alipo waambia: Huyu ni ngamia wa Mwenyezi Mungu, mwacheni anywe maji fungu lake. |
14. | Lakini walimkadhibisha na wakamchinja ngamia, kwa hivyo Mola wao Mlezi aliwaangamiza kwa sababu ya dhambi zao na akawafuta kabisa. |
15. | Wala Yeye haogopi matokeo yake. |