(SWAHILI) QURAN SURE SEÇİNİZ
(SWAHILI) QURAN |
95 - AT-TIN |
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
1. | Naapa kwa tini na zaituni! |
2. | Na kwa Mlima wa Sinai! |
3. | Na kwa mji huu wenye amani! |
4. | Bila ya shaka tumemuumba mtu kwa umbo lilio bora kabisa. |
5. | Kisha tukamrudisha kuwa chini kuliko walio chini! |
6. | Lakini wale walio amini na wakatenda mema, hao watapata ujira usio kwisha. |
7. | Basi ni kipi baadaye kitacho kukukadhibishia malipo? |
8. | Kwani Mwenyezi Mungu si muadilifu kuliko mahakimu wote? |