(SWAHILI) QURAN SURE SEÇİNİZ
(SWAHILI) QURAN |
| 93 - WADH-DHUH'AA |
| KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
|
| 1. | Naapa kwa mchana! |
| 2. | Na kwa usiku unapo tanda! |
| 3. | Mola wako Mlezi hakukuacha, wala hakukasirika nawe. |
| 4. | Na bila ya shaka wakati ujao utakuwa bora kwako kuliko ulio tangulia. |
| 5. | Na Mola wako Mlezi atakupa mpaka uridhike. |
| 6. | Kwani hakukukuta yatima akakupa makaazi? |
| 7. | Na akakukuta umepotea akakuongoa? |
| 8. | Akakukuta mhitaji akakutosheleza? |
| 9. | Basi yatima usimwonee! |
| 10. | Na anaye omba au kuuliza usimkaripie! |
| 11. | Na neema za Mola wako Mlezi zisimlie. |