1. |
Je! Imekufikia khabari ya msiba wa kufudikiza?
|
2. |
Siku hiyo nyuso zitainama,
|
3. |
Zikifanya kazi, nazo taabani.
|
4. |
Ziingie katika Moto unao waka -
|
5. |
Zikinyweshwa kutoka chemchem inayo chemka.
|
6. |
Hawatakuwa na chakula isipo kuwa kichungu chenye miba.
|
7. |
Hakinenepeshi wala hakiondoi njaa.
|
8. |
Siku hiyo nyuso nyengine zitakuwa kunjufu.
|
9. |
Zitakuwa radhi kwa juhudi yao,
|
10. |
Katika Bustani ya juu.
|
11. |
Hawatasikia humo upuuzi.
|
12. |
Humo imo chemchem inayo miminika.
|
13. |
Humo vimo viti vilivyo nyanyuliwa,
|
14. |
Na bilauri zilizo pangwa,
|
15. |
Na matakia safu safu,
|
16. |
Na mazulia yaliyo tandikwa.
|
17. |
Je! Hawamtazami ngamia jinsi alivyo umbwa?
|
18. |
Na mbingu jinsi ilivyo inuliwa?
|
19. |
Na milima jinsi ilivyo thibitishwa?
|
20. |
Na ardhi jinsi ilivyo tandazwa?
|
21. |
Basi kumbusha! Hakika wewe ni Mkumbushaji.
|
22. |
Wewe si mwenye kuwatawalia.
|
23. |
Lakini anaye rudi nyuma na kukataa,
|
24. |
Basi Mwenyezi Mungu atamuadhibu kwa adhabu iliyo kubwa kabisa!
|
25. |
Hakika ni kwetu Sisi ndio marejeo yao.
|
26. |
Kisha hakika ni juu yetu Sisi hisabu yao!
|