(SWAHILI) QURAN SURE SEÇİNİZ
(SWAHILI) QURAN |
99 - AZ-ZILZALAH |
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
1. | Itakapo tetemeshwa ardhi kwa mtetemeko wake! |
2. | Na itakapo toa ardhi mizigo yake! |
3. | Na mtu akasema: Ina nini? |
4. | Siku hiyo itahadithia khabari zake. |
5. | Kwa sababu Mola wake Mlezi ameifunulia! |
6. | Siku hiyo watu watatoka kwa mfarakano wakaonyweshwe vitendo vyao! |
7. | Basi anaye tenda chembe ya wema, atauona! |
8. | Na anaye tenda chembe ya uovu atauona! |